0

Kinda wa Azam FC, Farid Mussa huenda mambo yakawa mazuri kwake akiwa na umri mdogo kabisa.
Thomas Anderson raiwa Denmark amesema amepata taarifa za Farid akiwa nchini Uturuki na angependa kupata video yake ili aone kama inawezekana kumpeleka Ulaya.
Anderson ameitaja kampuni ya uwakawa wa wachezaji na kusema, anahitaji kujiridhisha kuhusiana na Farid kabla ya kwenda Azam FC.
“Nimepewa taarifa na makocha wa Hispania ambao wako kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Libya wakati Tanzania ilipocheza nao mechi mazoezi.
“Ninahitaji video zake kujiridshisha. Pia nimesikia amecheza mechi dhidi ya Nigeria kwa zaidi ya dakika 60. Napenda kupata video za mechi kadhaa,” alisema alipozungumza na SALEHJEMBE.
“Kama sitafanikiwa, nitaangalia kuhusiana na mahitaji yangu. Ninaweza kusafiri kuja tanzania pia nitapata nafasi ya kuzungumza na Azam FC,” alisisitiza.
Farid alionyesha kiwango kizuri hasa katika kipindi cha wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Libya ambayo ilikuwa ni ya mazoezi zilipokutana nchini Uturuki.
Lakini akaonyesha kiwango kizuri wakati Stars ilipokutana na Nigeria katika mechi ya kuwania kufuzu Afcon kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kinda huyo anakipiga Azam FC na amekuwa akiwaweka benchi wakongwe kwake akiwemo Simon Msuva ambaye ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara, msimu uliopita.

Post a Comment Blogger

 
Top