Akiongea na Bongo5 wiki hii Christian Bella amesema msanii kabla haujafanya show lazima utambue mashabiki wako huwa wanapenda kitu gani katika muziki wako.
“Mashabiki wana vitu vyao ambavyo wanataka kuvisikia au kuviona kutoka kwa msanii, unaweza ukawa na hit song kibao lakini ukashindwa kuzitumia. Kwa hiyo mimi binafsi tayari nimeshajua mashabiki wangu kwenye show huwa wanataka nini, ndo maana kila show ninayofanya lazima nifanye poa kwa sababu tayari nimeshajua nini wanataka mashabiki wangu,” alisema Bella.
Pia muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Nishike’ amewataka wasanii kuimba live na kwa hisia ili kuteka vizuri hisia za mashabiki wao
Post a Comment Blogger Facebook
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.