0
Polisi mjini Mwanga, mkoani Kilimanjaro umezuia msafara wa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa uliokuwa unaelekea Usangi kuhudhuria mazishi ya kada wa CCM, Peter Kisumo.

Vyanzo vya kuaminika toka mjini Mwanga vinasema, polisi walizuia msafara huo kutokana na kujumuisha idadi kubwa ya magari ya viongozi waandamizi wa Ukawa na wabunge wanaounda umoja huo jambo ambalo polisi hawakuafiki.Taarifa zinasema, tukio hilo lililotokea katikati ya Mwanga na Usangi lilizusha mjadala wa zaidi ya dakika 30, polisi wakitaka Lowassa aende mazishini peke yake huku magari mengine yaliyoambatana naye yarejee yalikotoka jambo ambalo halikuafikiwa na mwanasiasa huyo.Baada ya polisi kusisitiza kutoruhusu msafara mzima uende mazishini mgombea huyo aliamua yeye na maofisa wengine alioambatana nao kurudi Mwanga akisisitiza asingeweza kwenda peke yake akiwaacha watu aliambatana nao.

Post a Comment Blogger

 
Top