0
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akikimbia kuonesha ukakamavu kwenda jukwaani kujinadi wakati wa mkutano wa kampemi katika Uwanja wa Taifa mjini Ifakara wilayani Kilombero, Mkoa wa Morogoro jana.
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Mjini Ifakara, wilayani Kilombero, Morogoro. Dk Magufuli jana alifanya pia kampeni katika wilaya za Ulanga na Malinyi. Akihutubia kwa nyakati tofauti katika Wilaya za Ulanga, Malinyi na Kilombero, Dk Magufuli amesema kuwa akipta ushindi atawanyang'anya ardhi vigogo wote waliojilimbikizia ardhi bila kujiendeleza na kuigawa kwa wakulima na wafugaji nchiniMgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akijinadi akifanananisha upara wake na wa Mgombea Ubunge wa Jimbo jipya la Malinyi katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika Kata ya Mtimbila Wilaya mpya ya Malinyi, Morogoro. Dk Magufuli  alifanya pia kampeni katika wilaya za Ulanga na Kilombero. 
Mmoja wa wananchi akiwa na bango linalosema Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli anasubiri kuapishwa tu katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana Mjini Ifakara, wilayani Kilombero, Morogoro. Dk Magufuli alifanya pia kampeni katika wilaya za Ulanga na Malinyi.Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kilombero alipokuwa akitoka kufanya kampeni katika Wilaya za Ulanga na Malinyi kwenda   Mjini Ifakara, wilayani Kilombero, Morogoro.Mmoja wa wafuasi wa CCM akiwa na picha ya Dk Magufuli mjini Mahenge, wilayani UlangaWananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli mjini Mahenge, UlangaMadiwani wakinadiwa na Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni mjini Mahenge janaDk Magufuli akiombewa na mmoja wa masheikh baada ya kumaliza kujinadi kwa wananchi mjini Mahenge UlangaMgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akimpatia zawadi mtoto alipokuwa akiondoka mjini Mahenge wilayani Ulanga, baada ya kufanya mkutano wa kampeni.Wananchi waliouzuia msafara wa Dk Magufuli katika Kijiji cha Ilagua Mission, Wilaya mpya ya Malinyi ukielekea Kata ya Mtimbila.Moja ya mabango yaliyishikwa na wananchi katika mkutano wa kampeni katika Kata ya Mtimbila, wilayani Malinyi jana.Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Kata ya Mtimbila, wilayani Malinyi.Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Uratibu wa Msingi Wilaya ya Ulanga, Evance Tagala akionesha kadi kabla ya kuikabidhi kwa Dk Magufuli alipotangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo wa kampeni katika Kata ya Mtimbila.Wananchi wakimsikiliza Dk Magufuli alipokuwa akijinadi katika Kijiji cha Lupilo wilayani Ulanga.Sehemu ya umati wa watu wakati wa kampeni CCM kwenye Uwanja wa Taifa, Ifakara wilayani Kilombero, Morogoro , uliohutubiwa na Mgombea urais wa CCM, Dk John MagufulMwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee wa CCM, Abdalah Bulembo  akizungumza maneno ya kumnadi Dk Magufuli kabla ya kumkaribisha kujinadi wakati wa mkutano wa kampeni mjini Ifaraka

Post a Comment Blogger

 
Top