0
Mgombea Urais wa ACT Mhe Khamis Iddi Lila akiwasili katika viwanja vya Afisi ya Tume ya Uchaguzi ziliko katika hoteli ya Bwawani Zanzibar kwa ajili ya kurejesha famu yake ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT. Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT Mhe Khamis Iddi Lila akiwa na mkoba wake wa fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar akishindikizwa na Viongozi wa Chama hicho wakiwasili katika Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC bwawani Zanzibar. Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT Mhe Khamis Iddi Lila akiwa na Viongozi wa Chama hicho wakati wa kurejesha Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar. Wanachama wa Chama cha ACT wakiwa katika ukumbi wa Tume wakimshindikiza Mgombea wao wa Urais wa Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo.

Post a Comment Blogger

 
Top