0
Siku chache mara baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa Kujiuzulu na kuamua kuachana na siasa kutokana na kutokuridhishwa na utendaji ndani ya chama hicho baadhi ya vijana wamezidi kukihama chama hicho jambo ambalo linadaiwa kukidhoofisha chama hicho.
Baadhi ya vijana mjini Tabora waliokuwa wanachama wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA wameandamana hadi ofisi ya CCM Wilaya na kudai wanajiunga na chama hicho baada ya kugundua kasoro za baadhi ya Viongozi wa Ukawa.
Wamesema wamegundua wamepotea baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dokta Wilbroad Slaa kuelezea mapungufu yaliyojitokeza katika kuwakaribisha na kuwapitisha wagombea mbalimbali wa chama hicho.
Vijana hao ambao wanadai kumuunga mkono Slaa wanadai kuguswa na maneno yaliyotolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dk Wilbroad Slaa hivyo kuamua kukihama chama hicho.
Vijana hao mbali licha  ya kuvihama vyama vyao,pia walichana kadi mbele ya ofisi ya Chama cha Mapinduzi,wakidai kuchoshwa na vyama vya upinzani.

Post a Comment Blogger

 
Top