0
Baadhi ya vijana waliodai kuwa wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA mkoani Arusha wameandamana na kuchoma moto bendera na kadi za vyama vyao wakidai kumuunga mkono aliyekuwa katibu Mkuu wa CHADEMA Dokta Wilbroad Slaa aliyetangaza kuachana na siasa.

Wanachama hao wengi wao wakiwa vijana waliokuwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali wamedai kuachana rasmi na vyama vinavyounda ukawa na badala yake wanajiunga na chama cha ACT-Wazalendo.
Baadhi ya wanachama hao akiwemo Hassan Abdala na Rajabu Mshana ambao awali wanadai kuwa wafuasi wa vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF wamesisitiza kuwa hawako tayari kuendelea kuviunga mkono vyama hivyo kwa sababu vimeonyesha wazi kutokuwa na ajenda ya kuwasaidia watanzania maskini.
Uongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo kupitia kwa mwenyekiti wake wa Mkoa wa Arusha Etomih Malla umesema upo radhi kuwapokea wanachama wapya lakini ukiwataka wajitokeze kukiunga mkono hususani kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Harakati hizo zimeibuka wakati ambapo siku chache zilizopita aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema Dakta Wilbroad Slaa alitangaza rasmi kuachana na masuala ya siasa.
  SOURCE ; STAR TV

Post a Comment Blogger

 
Top